Jumanne, 15 Aprili 2014

WANAUME NA MITINDO YA NYWELE.



Habari za asubuhi wapendwa wasomaji wa blog hii natumaini tupo wazima  tumshukuru Mungu kwa yote na tuwaombee wale walio athirika na mafuriko waweze kupato sehemu ya kuishi na waendelea na shughuli zao.


Siku ya leo nitazungumzia kuhusu Mtindo ya  Nywele kwa wanaume  inavyoweza kumfanya mtu aonekane tofauti, Kuna aina mbali mbali ya mtindo ya nywele kwa wanaume  kuna wanaume wanapenda kunyoa mitindo  mbali mbali  ya nywele na kuna wengine wanapenda kusuka mitindo mbali mbali.

Hizi ni baadhi ya mitindo mbali mbali ya nywele:


 Mtindo huu unapendwa na wanaume wanaopenda kusuka aina tofauti tofauti za nywele.Sio wanaume wote wanapenda kusuka nywele,ila wanaume wengine wanapenda sana kusuka mitindo mbali mbali ya nywele na moja wapo ni huo mtindo hapo juu.




Moja wapo ya mtindo wa nywele unaopendwa sana na wanaume wengi sana wanapenda kunyoa style hii ya nywele ambayo inaitwa kama ( kiduku) ni style ambayo haiwezi kuisha fashion kuliko style nyingine za nywele.




Style nyingine ya nywele kwa wanaume ambao wanapenda kusuka nywele zao kwa kuchanganya na lasta na kuweka vishanga kwenye nywele zao, kama unavyoona kwenye picha hapo juu.



Jumatatu, 14 Aprili 2014

WANAUME NAO HATUWASAHAU KATIKA KUPENDEZA NA VITENGE

Habari za asubuhi  msomaji wa blog hii, tumuombe Mungu atujalie hali ya hewa iweze kubadilika  maana asilimia kubwa ya watu  tumeathirika na mvua kubwa ilio nyesha kwanzia ijumaa hadi jumamosi .


Siku ya leo nitazungumzia kuhusu vazi la kitenge kwa Wanaume kuonekana tofauti na wenye kuvutia mda wote. Vazi la kitenge kwa wanaume linaweza kushonwa kama suti na mtindo mbali mbali.

Hizi ni baadhi ya picha za wanaume wakiwa wamevaa suti za kitenge.
Hili ni moja wapo ya vazi la kitenge muundo wa suti.






Sio wanaume wote vakivaa vazi hili wanavutia  unatakiwa kwa kuangalia umbo lako kwanza sio umemuona mtu amevaa na we unaenda kushona vazi kama hili.

Tukiangalia hizo picha hapo juu imeonesha models wakiwa wamevaa vazi hili wakiwa si wanene sana  wana umbo la kawaida, lakini si mtu uwe mnene sana  halafu unavaa vazi hili cha kuzingatia kwanza angalia umbo lako je litafaa kwenye vazi hili.




Na hili ni moja wapo ya mtindo wa vazi la kitenge  linalo pendeza sana, unaweza kushona mitindo mbali mbali ya kitenge ikiwemo kushona kaptura kama unavyo apo juu kwenye picha.



Jumatano, 9 Aprili 2014

MAVAZI YA OFISINI

Habari  zenu Wapendwa, tumshukuru Mungu kwa kuiona tena siku hii ya leo, Mpenzi msomaji wa blog hii nakukalibisha kwa mara nyingine tena  usisite kutoa maoni yako  karibu sana.



Siku ya leo nitazungumzia kuhusu Mavazi ya ofisini  ni mavazi ya aina gani? siku ya leo utaweza kuyafahamu kwa undani zaidi , msomaji  mwavazi ya ofisini ni mavazi yanayo heshimika sana  mtu hawezi kuvaa jinzi au  suluali ya jinzi  kwa upande wa wasichana na wanawake hilo sio vazi la ofisini ingawa asilimia kubwa  wana vaa bora  amekwenda ofisini. Lakini ofisini ni sehemu muhimu sana kwa kuvaa vazi la heshima . haya ni baadhi ya mavazi ya ofisini  yanavyo leta muonekano tofauti.
Hili  ni moja wapo ya vazi la ofisini  linalo leta muonekano  tofauti kwa wavaji,pia rangi nyeupe na nyeusi ni moja wapo ya rangi zinazo leta mvuto na inapendeza kwa  kila mtu.




Rangi  ya  Blue na black ni rangi inayovutia sana kwenye mavazi ya suti   wadada wengi wanapenda sana kuvaa aina hii ya rangi.


Tumeweza kuyaona baadhi ya mavazi ya Ofisini yanavyo mfanya mtu awe tofauti hata mtu akivaa vazi la suti akawa anaenda sehemu nyingine tofauti na ofisini,anaonekana tu kama anafanya kazi. Kama tulivyo yaona mavazi ofisini  ni mavazi yanayo heshimiwa sana.





Muonekano tofauti



Mpenzi msomaji hayo yalikuwa ni mavazi ya ofisini, tuangalie upande mwingine wa Viatu pamoja mikoba inayo faa kuvaa kwenye mavazi ya ofisini na kumfanya mvaaji aonekane wa tofauti.


 Kwa upande wa  Viatu


 
inapendeza sana kwenye vazi la suti ukiwa umevaa vazi la black na white inavutia sana




Kwa wale wakinadada na wakina mama wanaoweza kutembelea viatu vya juu kama nilicho kuonesha hapo juu ni moja wapo ya kiatu kinacho pendeza sana , ila kina faa kwa wale wenye magari yao sio unapanda daradara ukiwa umevaa kiutu kama hiki.

Kwa upande wa pochi

  Ni pochi gani inafaa kuvalia nguo za suti












Hizi ni baadhi ya pochi zinazo leta mvuto kwa wanawake na wasichana  na kwa upande wa mavazi ya siti. Mpenzi msomaji wa blog hii utakuwa umeweza kuyaona mavazi ya ofisini pamoja na pochi na  viatu , msomaji endelea kuwa nami katika blog hii karibu sana


 hapo hupo msomaji ina pendeza sana
karibu sana. 

Jumanne, 8 Aprili 2014

MAVAZI YA USIKU

Habari  zenu Wapendwa tumshukuru Mungu kwa  kutupa pumzi siku hii ya leo, Mpenzi msomaji katika Blog hii usisite kutoa ushauri na comments katika Blog hii  karibu.


Mpenzi msomaji siku ya leo natazungumzia kuhusu mavazi ya usiku  yanatakiwa kuvaliwa sehemu gani? na wakati gani? Watu wengi wamekuwa hawafahamu nguo ya usiku ni nguo ya namna gani?kwa siku ya leo utaweza kufahamu  nguo mbali mbali.


Wanawake wengi pamoja na wasichana wamekuwa wakivaa nguo za kungaa mchana kwanye jua kali ambayo si muda maharumu wa kuvaa vazi hilo , Muda maarumu wa kuvaa vazi hilo ni usiku uwe unaenda  kwenye harusi, au sherehe yoyote hile.Hizi ni baadhi ya mavazi ya usiku.
Haya ndio baadhi  ya mavazi ya usiku na yanayo leta mvuto na unadhifu pale tu unapo vaa vazi hili la usiku . Pia wasichana wengi  pamoja na wanawake wanapenda kuvaa nguo  za rangi rangi kama rangi ya njano,orange  hizi rangi zinawaka sana ingawa wakina dada wengi huzivaa mchana inakuwa haipendezi kwa mtoko wa mchana inafaa kwa mtoko wa usiku unakuwa  mtu wa kuvutia.

Alhamisi, 3 Aprili 2014

NGUO NDEFU KWA MTOKO INAPENDEZA PIA

Habari zenu wapendwa  wasomaji wa blog hii ya mitindo  ambayo ipo kwa ajili yako msomaji, usisite kutoa mawazo yako ,ushauri.

 Siku ya leo nitazungumzia kuhusu umuhimu wa kuvaa nguo ndefu hasa wakati wa kwenda kwenye mtoko wa halfa iwe usiku au mchana,kwani wa kinadada wengi wameonekana kuvaa nguo fupi wanapotoka jambo ambalo limejenga umaarufu kuliko nguo ndefu.
Hata hivyo wengi wamekuwa wakipenda sana  ingawa wengi wao wamesahau kuwa hata nguo ndefu ina umuhimu wakr hasa kataka mambo ya halfa za usiku kwani mara nyingi huwa zinawafanya, wavaaji kuonekana katika hali fulani ya urembo ukiachilia mbali kuwa vazi lefu pia huleta heshaima kutokana  na Mla na desturi zetu Watanzania.
Hayo ni baadhi ya nguo ndefu kwaajili ya mtoko






Mpezi msomaji hayo ni baadhi tu ya mavazi yanayo onesha mvuto,na kuwa nadhifu mda wote na unaweza kwenda sehemu yoyote kuliko yule alie vaa nguo fupi anakuwa hayupo huru ,ila yule alie vaa nguo ndefu anakuwa huru mda woto.






Jumatano, 2 Aprili 2014

VAA VAZI LA KITENGE UONEKANE TOFAUTI

Habari zenu Wapendwa  wasomaji wa safu hii ya urembo ambayo huwa inakujia kila siku  iliwa maalumu kwa ajili yako  urembo wako  wewe Mwanadada na hata kupeana ushauri katika mtindo mbalimbali kuonekana nadhifu wakati wote.
     
Siku ya leo nitazungumzia kuhus vazi la kitenge  linavyo mfanya mtu aonekane tofauti wakati wote, miongoni mwa vazi ambalo  awali lilikuwa halipewi nafasi kubwa na vijana tofauti na ilivyo sasa na umaafufu wake unazidi kushika kasi.


Vijana wengi wenye umri kati ya miaka 15na 30, wanahisi kupoteza mvuto wao wavaapo vazi la kitenge.Hata hivyo hali hiyo hutokana na fikra kuwa aina hiyo ya nguo inawafaa  zaidi wanawake wenye umri mkubwa.


Hilo ni miongoni mwa vazi la kitenge linalo mfanya mvaaji aonekane nadhifu na tofauti.

Wengi wamekuwa wakifikiria kwamba kitenge kinaweza kuvaliwa kanisani au katika maeneo yanayokusanya watu wa heshima pekee kama vile mikutano,semina, warsha au ofisini.
Hivyo ni kasumba iliyotawala vijana hasa wasichana walio wengi, bila kufahamu ukweli kwamba kitenge kinaweza kuwa maalumu kwa ajili yao, endapo kitashonwa  na kutengezwa nguo itakayozingatia mazingira ya eneo husika.
Ni wazi kwamba kitenge kinaweza kushonwa katika mitindo mbalimbali inayoweza kumfanya mvaaji kuonekana nadhifu.Miongoni mwa mitindo hiyo ni vazi la kitenge inayoweza kuvaliwa mahali popote .
Kwa kutumia fundi mwenye uwezo na ubunifu,kitenge kinaweza kubuniwa katika mitindo mbalimbali ya gauni , sketi na brauzi na mitindo mingine mingi itakayomfanya mvaaji kujivunia zazi hilo hata kuonekana tofauti na watu wengine.
Hizo ni baadhi ya picha zinazo onesha mitindo mbalimbali ya kitenge, Mpenzi msomaji usisite kulike,share na pia kuto maoni yako .


Mpenzi msomaji karibu katika blog hii inayoitwa ulimbwende wa mitindo ni blog ambayo itazungumzia masuala yote ya mitindo ya kike pamoja na ya kiume pia na vipodozi vya  aina zote pamoja matumizi yake. Napenda kuwakaribisha wapenzi wasomaji wa blog hii kunipa maoni na kunirekebisha pale nitakakopuwa nimekosea.



Karibuni sana