Jumatano, 2 Aprili 2014

VAA VAZI LA KITENGE UONEKANE TOFAUTI

Habari zenu Wapendwa  wasomaji wa safu hii ya urembo ambayo huwa inakujia kila siku  iliwa maalumu kwa ajili yako  urembo wako  wewe Mwanadada na hata kupeana ushauri katika mtindo mbalimbali kuonekana nadhifu wakati wote.
     
Siku ya leo nitazungumzia kuhus vazi la kitenge  linavyo mfanya mtu aonekane tofauti wakati wote, miongoni mwa vazi ambalo  awali lilikuwa halipewi nafasi kubwa na vijana tofauti na ilivyo sasa na umaafufu wake unazidi kushika kasi.


Vijana wengi wenye umri kati ya miaka 15na 30, wanahisi kupoteza mvuto wao wavaapo vazi la kitenge.Hata hivyo hali hiyo hutokana na fikra kuwa aina hiyo ya nguo inawafaa  zaidi wanawake wenye umri mkubwa.


Hilo ni miongoni mwa vazi la kitenge linalo mfanya mvaaji aonekane nadhifu na tofauti.

Wengi wamekuwa wakifikiria kwamba kitenge kinaweza kuvaliwa kanisani au katika maeneo yanayokusanya watu wa heshima pekee kama vile mikutano,semina, warsha au ofisini.
Hivyo ni kasumba iliyotawala vijana hasa wasichana walio wengi, bila kufahamu ukweli kwamba kitenge kinaweza kuwa maalumu kwa ajili yao, endapo kitashonwa  na kutengezwa nguo itakayozingatia mazingira ya eneo husika.
Ni wazi kwamba kitenge kinaweza kushonwa katika mitindo mbalimbali inayoweza kumfanya mvaaji kuonekana nadhifu.Miongoni mwa mitindo hiyo ni vazi la kitenge inayoweza kuvaliwa mahali popote .
Kwa kutumia fundi mwenye uwezo na ubunifu,kitenge kinaweza kubuniwa katika mitindo mbalimbali ya gauni , sketi na brauzi na mitindo mingine mingi itakayomfanya mvaaji kujivunia zazi hilo hata kuonekana tofauti na watu wengine.
Hizo ni baadhi ya picha zinazo onesha mitindo mbalimbali ya kitenge, Mpenzi msomaji usisite kulike,share na pia kuto maoni yako .


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni