Jumanne, 15 Aprili 2014

WANAUME NA MITINDO YA NYWELE.



Habari za asubuhi wapendwa wasomaji wa blog hii natumaini tupo wazima  tumshukuru Mungu kwa yote na tuwaombee wale walio athirika na mafuriko waweze kupato sehemu ya kuishi na waendelea na shughuli zao.


Siku ya leo nitazungumzia kuhusu Mtindo ya  Nywele kwa wanaume  inavyoweza kumfanya mtu aonekane tofauti, Kuna aina mbali mbali ya mtindo ya nywele kwa wanaume  kuna wanaume wanapenda kunyoa mitindo  mbali mbali  ya nywele na kuna wengine wanapenda kusuka mitindo mbali mbali.

Hizi ni baadhi ya mitindo mbali mbali ya nywele:


 Mtindo huu unapendwa na wanaume wanaopenda kusuka aina tofauti tofauti za nywele.Sio wanaume wote wanapenda kusuka nywele,ila wanaume wengine wanapenda sana kusuka mitindo mbali mbali ya nywele na moja wapo ni huo mtindo hapo juu.




Moja wapo ya mtindo wa nywele unaopendwa sana na wanaume wengi sana wanapenda kunyoa style hii ya nywele ambayo inaitwa kama ( kiduku) ni style ambayo haiwezi kuisha fashion kuliko style nyingine za nywele.




Style nyingine ya nywele kwa wanaume ambao wanapenda kusuka nywele zao kwa kuchanganya na lasta na kuweka vishanga kwenye nywele zao, kama unavyoona kwenye picha hapo juu.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni