Jumatatu, 14 Aprili 2014

WANAUME NAO HATUWASAHAU KATIKA KUPENDEZA NA VITENGE

Habari za asubuhi  msomaji wa blog hii, tumuombe Mungu atujalie hali ya hewa iweze kubadilika  maana asilimia kubwa ya watu  tumeathirika na mvua kubwa ilio nyesha kwanzia ijumaa hadi jumamosi .


Siku ya leo nitazungumzia kuhusu vazi la kitenge kwa Wanaume kuonekana tofauti na wenye kuvutia mda wote. Vazi la kitenge kwa wanaume linaweza kushonwa kama suti na mtindo mbali mbali.

Hizi ni baadhi ya picha za wanaume wakiwa wamevaa suti za kitenge.
Hili ni moja wapo ya vazi la kitenge muundo wa suti.






Sio wanaume wote vakivaa vazi hili wanavutia  unatakiwa kwa kuangalia umbo lako kwanza sio umemuona mtu amevaa na we unaenda kushona vazi kama hili.

Tukiangalia hizo picha hapo juu imeonesha models wakiwa wamevaa vazi hili wakiwa si wanene sana  wana umbo la kawaida, lakini si mtu uwe mnene sana  halafu unavaa vazi hili cha kuzingatia kwanza angalia umbo lako je litafaa kwenye vazi hili.




Na hili ni moja wapo ya mtindo wa vazi la kitenge  linalo pendeza sana, unaweza kushona mitindo mbali mbali ya kitenge ikiwemo kushona kaptura kama unavyo apo juu kwenye picha.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni